Uhamisho/Exil

Publié le par SLAM POESIE DE FAUSTINE

 

Hilo ndilo neno zuri sana,

Kawa kutamka ghaibu,

Upweke,

Umbali ambao haushikiki

Uhamisho, hilo ndilo neno zuri sana,

 

Kwa kuwauliza watu tunaopenda,

Mko wapi ?

Kwa kuwauliza watu tunaopenda,

Kwa nini nilichagua,

Njla ya mawazo ?

Kwa nini niliondoka ?

Kwa nini niliikimbia nchi yangu iliyofukarika ?

 

Uhamisho,

Hilo ndilo neno zuri sana,

Kuficha huzuni,

Ya dunia yenye mbio kubwa,

Bila uzuri.

 

Uhamisho unamaanisha hamu na mambo yaliyozoewa,

Uhamisho unamaanisha utofauti,

Uhamisho unamaanisha kuwa hatukupokelewa,

Kuwa tunastahamiliwa tu.

 

Uhamisho no neno zuri sana,

Lakini lenye kuadhibisha,

Kwa sabatu tutapata ujoto wa titi la mama wapi,

Tukihama,

Hata kwetu ?

 

Uhamisho tunaogopa,

Uhamishoni tuna njaa,

Uhamishoni tunahisi baridi,

Uhamishoni hatukuwa kitu chochote.

 

Uhamisho ni shimo lisilo mwisho,

Uhamisho ni kisima bila kikomo,

Uhamisho unamaanisha kuwa tamaa iliktwa,

Uhamisho unamaanisha kuwa wakati ujao ni machweo,

Na hata kama jua linang'aa,

Mtu aliyehama anabaki gizani.

 

Uhamisho unamaanisha,

Kuwa sigawi,

Furaha zenu na shida zenu,

Uhamisho unamaanisha,

Kuwa hamwezi,

Kushahidia zangu.

 

Uhamisho ni neno zuri sana,

Kukuita katika usiku,

Kusema kwamba hata,

Nikipiga kelele, nikilia, nikiomba,

Hakuna kitu kutuepusha na

Huo ambao ndio usiku mrefu mno.

 

 

Traduit en swahili par Mathieu Roy de l'Ouganda

Texte original de Faustine Lima

Pour être informé des derniers articles, inscrivez vous :

Commenter cet article